- Bilal Philips
- islamhouse.com
- 2011
- 72
- 5999
- 3904
- 2388
Ujumbe wa kweli wa Yesu Kristo
yesu Kristo anawakilisha akiwa ni kiungo cha kuunganisha baina ya dini mbili zenye wafuasi wengi zaidi duniani leo hii; Ukristo na Uislamu.
Somo lifuatalo, linalohusu Ujumbe wa Yesu na Haiba yake limeegemea katika kiungo hicho.
Inatarajiwa kuwa, kwa kupitia somo hili, wote wawili; Waislamu na Wakristo watafahamu vizuri ukuu wa Yesu na umuhimu wa ujumbe wake.
Hata hivyo, ili tuutambulishe barabara ujumbe wa kweli wa Yesu Kristo, mtazamo usio na upendeleo ulibidi udumishwe katika kipindi cha kufanya uchunguzi wetu. Hisia zetu zisiruhusiwe kuweka kiwingu kwenye uoni wetu na kwa hiyo, kutupofua tusiuone ukweli. Lazima tuyatazame masuala mazima kimantiki na tuutenganishe ukweli uepukane na uongo kwa msaada wa Mungu Mwenye nguvu.
Source: islamhouse.com