- Department of Fatwa
- Department of Fatwa State of Kuwait
- 2017
- 362
- 6936
- 3763
- 2666
MWONGOZO WE NYE FAIDA WA SHERIA ZA KIISLAMU KWA MUISLAMU MPY
Shukurani zote ni za Allah Mola wa viumbe, na nakiri kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa ila Allah pekee, asiye na mshirika, kipenzi cha watu wema. Na nakiri kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake.
Tunaomba rehema na amani zimfikie yeye, Familia yake na Swahaba wake wote.
Ama baada ya haya: Hakika, neema za Allah kwa mwanadamu ni nyingi na kubwa. Hazihesabiki na hazidhibitiki.
Allah anasema kuwa:
“Na mkihesabu neema za Allah hamtaweza kuzidhibiti. Hakika, Allah ni mwingi wa kusamehe (na) mwingi wa kurehemu”. Sura Annahl:18.
Neema kubwa na adhimu kabisa miongoni mwa neema za Allah ni kumuwezesha mja kufuata njia yake iliyonyooka, dini yake ya haki ambayo ameiridhia na kuwaamrisha watu kuifuata.
Allah amesema kuwa:
“Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu, na nimeridhia kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu”. Sura Almaida: 3.
Hakika, hiyo ni neema kubwa na zawadi kubwa ambayo mwanadamu ameneemeshwa.
Kwa neema hiyo, inapatikana raha na wema duniani na inapatikana nusura na kufaulu kukubwa Akhera.
Allah amesesema kuwa:
“Kwa yakini, walioamini na kufanya vitendo vizuri makazi yao yatakuwa pepo za Firdausi wakikaa milele humo. Hawatataka kuondoka katika makazi hayo”. Sura Al- kahf: 107-108.
Department of Fatwa State of Kuwait